MAMLAKA YA MAJI SAFI
NA MAJI TAKA TANGA UWASA, IMEDHAMIRIA KUONGEZA WINGI NA UBORA WA MAJI YANAYOSAMBAZWA
NA MAMLAKA HIYO MKOANI HUMO
.
Mamlaka hiyo ambayo hadi sasa imefanikiwa kusambaza maji safi kwa asilimia 94.5 na kusema kuwa
imefanikiwa kupunguza kiwango cha maji taka na kufikiai asilimia 9.4 hadi sasa kwa
wateja wa jiji hilo.
Wamesema kuwa hii inatokana na mamlaka hiyo kufahamu umuhimu
wa kutoa huduma bora kwa wateja wake sambamba na mikakati iliyojiwekea katika
kuhakikisha inaendana na ongezeko la watumiaji wake na kuondoa uhaba wa maji
mkoani Tanga.
Imesema hilo litawezekana kwa kuwa tayari imeshaanza ujenzi
wa maeneo ya kusafishia maji taka hasa Muheza na Nachingwea,wakati huohuo
inaandaa eneo la Utofu lengo likiwa hilo hilo la upatikanaji wa maji safi,jambo
litakalo ongeza wingi wa maji safi,wakati huohuo kuondoa kabisa upungufu wa
maji, ambapo hadi kufikia sasa mamlaka hiyo inazalisha meta za ujazo 27,740 kwa
siku na kukidhi mahitaji ya wateja wake
.
Kuhusu upotevu wa maji, kwa maana ya matumizi yasiyosahihi
yanayofanywa na baadhi ya wateja wake,aidha
kwa kutofahamu au kwa makusudi, kupasuka kwa mabomba katika maeneo yaliyokuwa
vigumu kuyatambua haraka, mamlaka imesema itahakikisha itaondoa kadhia hiyo,
lakini pia itawashirikisha moja kwa moja wananchi,mpaka sasa imefanikiwa
kupunguza upotevu huo kutoka asilimia 25.9 hadi asilimia 23
.
Maelezo hayo yametolewa na mhandisi wa maji mkoani Tanga bwana Chales Alam
katika kikao cha baraza la madiwani liliofanyika katika ukumbi wa jiji hilo
ambapo mamlaka ya maji safi na maji taka Tanga UWASA na Shirika la umeme
Tanzania TANESCO walikuwa waalikwa.
Aidha amesema kuwa hadi sasa mamlaka hiyo imefanikiwa kuwa
mamlaka bora Tanzania katika utendaji kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine ya
nyuma.
Mbali na mafanikio waliyoyapata lakini pia kuna changamoto
mbalimbali zinazochangia kukwamisha baadhi ya malengo kwa mamlaka hiyo kua ni
uchakavu wa miundombinu ya maji safi na taka iliyojengwa tangu mwaka
1940,kutegemea chanzo kimoja cha maji cha mto zigi,uchafuzi na uharibifu wa
chanzo cha maji kwa watu kuendesha shughuli za kilimo,ukataji miti,uchimbaji wa
madini na kadhalika.
Amezitaja changamoto zingine kuwa uharibifu na wizi wa
miundo mbinu ikiwemo meta za maji,wateja wasio waaminifu(wizi wa maji),uwezo
mdogo kifedha katika kufanikisha miradi ya kuboresha huduma(kutanua na
kukarabati miundombinu),chanzo kimoja cha nishati ya umeme kutoka TANESCO,
wateja kutolipa kwa wakati ,akitolea mfano taasisi za UMMA.
Amesema ili kuondoa changamoto ya nishati ya umeme mamlaka
kushirikiana na benki ya dunia itanunu jenereta kwa ghalama ya shilingi bilioni
moja,watabadilisha bomba chakavu katika maeneo mbalimbali yenye urefu wa KM 1,200
hadi 2017,kujenga chemba 15 ili kuongeza uzalishaji wa maji taka,sambamba na
kuongeza makusanyo kutoka asilimia 94.5 hadi 99 ya wakazi wa jiji kwa maji safi
kutoka 9.4% hadi 9.7% kwa maji taka ifikapo june 2017.
CHALS,
amesema mipango ya UWASA kwa sasa ni ukarabati wa majengo,ununuzi wa ardhi kwa
ajili ya ujenzi wa matanki na upanuzi wa huduma, sanjari na uboreshai wa TEHAMA
yaani kulipia kwa njia ya simu,itakayosaidia upatikanaji wa huduma kwa haraka
na ufanisi,ili hayo yote yaweze kufikiwa
mamlaka inahitaji zaidi ya bilioni 424 katika kipindi cha miaka 3,ambo
kwa sasa mamlaka hiyo inakusanya shilingi 7.2bilioni kwa mwaka,lakini
wanampango wa kuanza kutumia meter za Pre-paid kwa kuanzia kwa wateja wachache hasa wateja sugu.


0 comments:
Post a Comment