MBUNGE
wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau
amehaidi kushirikiana na Uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani kuhakikisha
kinapatikana chumba na vifaa vya kutosha kwa ajili ya watoto wanaozaliwa chini
ya umri.
Mwidau ameyasema hayo wakati alipokuwa
akikabidhi jengo alilolijenga kwenye hospitali hiyo lililogharimu kiasi chashilingi milioni tano kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani, Dennis Naromba kwa
ajili ya kupumzikia wagonjwa na ndugu zao wakati wakisubiri taratibu za kupatiwa
matibabu.
Amesema kuwa kimsingi hawezi kuvumilia kuona
watoto wanaozaliwa chini ya umri wanapoteza maisha kutokana na ukosefu wa
chumba hicho wakati tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi wa kina ili kuweza
kulimaliza.
Akielezea changamoto hiyo, Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya wilaya, Dennis Naromba amesema ukosefu wa chumba chenye vifaa
vya kutosha kwa ajili ya kuwahifadhia watoto waliozaliwa chini ya umri ni moja
ya
changamoto zinazosababisha vifo vya watoto wenye
umri chini ya miaka mitano.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Jengo hilo,
Mbunge Mwidau amesema kuwa changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa sana kwa wagonjwa
waliokuwa wakienda kupata matibabu wakiwa na ndugu zao kutokana na kutokuwepo
eneo la wao kupumzika kwa ajili ya kusburi
taratibu nyengine.
Amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo
mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya hospitali hiyo walimpa taarifa ya kuwepo kwa
tatizo hilo na hivyo akaona umuhimu wa kusaidia jambo hilo kupitia Mfuko wake
wa
Mwidau Foundation ili kuweza kulipatia ufumbuzi
jambo hilo.
Aidha amesema kuwa kwa sababu ni jambo hilo ni
nzuri kwa sababu lina igusa nzima ya wana pangani hivyo waliutumie vizuri kwa
ajili ya mapumziko yao wakati wanapokwenda kwenye hospitali hiyo kupata
matibabu wakiwa na ndugu zao


0 comments:
Post a Comment