![]() |
| MAELFU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO |
Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi
ya aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Afrika Kusini Senzo Meyiwa
yanayofanyika jijini Durban.
![]() |
| WAKATI WA UHAI WAKE AKIONESHA UMAHIRI WAKE |
Meyiwa, mwenye umri wa miaka 27,
alipigwa risasi Jumapili iliyopita, baada ya majambazi kuingia nyumbani
mwa mpenzi wake karibu na Johannesburg.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa
alifikishwa mahakamani Ijumaa na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda
mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.
Kifo cha Meyiwa
kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha
kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.
Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.
Senzo Meyiwa alionekana kama kivutio katika mchezo wa mpira miongoni mwa wananchi wa Afrika Kusini.
Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.
Mazishi
ya mwanamichezo mwingine shujaa wa Afrika Kusini, bingwa wa zamani wa
dunia wa mbio za mita 800 Mbulaeni Mulaudzi, pia yatafanyika Jumamosi.
Mulaudzi aliuawa katika ajali ya gari kabla ya kifo cha Meyiwa.
Bendera nusu mlingoti
Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.
Mechi kati ya timu za Orlando Pirates na Kaiser Chiefs katika ligi ya Afrika Kusini imeahirishwa baada ya kifo cha Meyiwa.
Senzo Meyiwa alikuwa nahodha na mlinda mlango wa timu ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.
Mamlaka
ya soka nchini humo wametangaza mchezo wa timu ya taifa ya Afrika
Kusini wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan
ifanyike Durban.
Polisie wamesema Ijumaa kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.
Mtuhumiwa
huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na
mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa
kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11.Polisi wametangaza zawadi
kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio
hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.




0 comments:
Post a Comment