Mbunge wa jimbo la tanga mjini Mh Omari r Nundu , ameitaka halmashauri
ya jiji la tanga
kuhakikisha inawatengea vijana na akina mama pesa za halmashauri zilizotakiwa zitengwe kuanzia mwaka 1993 ambapo kwa mkoa wa Tanga zimetolewa miaka mitatu tu, huku miaka18 iliyofuata hazikutolewa au kutokutengwa kabisa.
kuhakikisha inawatengea vijana na akina mama pesa za halmashauri zilizotakiwa zitengwe kuanzia mwaka 1993 ambapo kwa mkoa wa Tanga zimetolewa miaka mitatu tu, huku miaka18 iliyofuata hazikutolewa au kutokutengwa kabisa.
Mh. Nundu ambae anatumia ahadi ya 4 na 8 za chama cha
mapinduzi katika kuliendesha jimbo la tanga amewataka vijana kutokudanganywa
kuwa yeye ndie anayezuia mikopo hiyo isitoke badala yake amewataka vijana na
akina mama wa mkoa wa tanga kuchangamkia fursa hiyo ambayo ni ya
kila kijana bila kujali itikadi za vyama.
kila kijana bila kujali itikadi za vyama.
Aidha Mh.nundu alifika mbali zaidi kwa kuwataka vijana
wajijengee kuaminika mara watakapopata mikopo hiyo kwa kuhakikisha wanaitumia
kwa malengo.
Itakumbukwa kuwa
Mbunge Omari Rashidi Nundu ,alisamehe mshahara wake wa miaka mitano zaidi
ya shilingi milioni 111 kwa kuwakopesha wakazi wa Watanga ili wajikwamue
kiuchumi na waondokane na lindi la umasikini uliopo mkoani hapa,pamoja na
juhudi hizo,lakini pesa hizo zilirudi
milioni nane tu, na idadi kubwa ya waliokopeshwa wakishindwa kuzirudisha
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo watu wanaopita wakisema pesa za mbunge
huyo zilikuwa za misaada.
Mbunge omar nundu anabaki kuwambunge wa kwanza katika historia ya mkoa wa tanga kusamehe mshaharawake kwa ajili ya kuwakomboa wananchi,amesema pamoja na hayo yote kutokea lakini bado wananchi hao wanafursa ya kukopa,akitolea mfano Benki ya Posta,kwakuwa Benki hiyo kuwa na riba isiyowaumiza wananchi.



0 comments:
Post a Comment