![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai |
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Mafisa
Kata ya Mvungwe Tarafa ya Mgera wilayani Kilindi ameuawa kwa kuchomwa na kitu
chenye ncha kali sehemu ya Tumboni, Shingano na Kichwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Fresser Kashai amethibitisha kutokea tukio hilo ambalo lilitokea Octoba 7 mwaka
huu saa 11:30 wakati Marehemu akiwa shambani kwenye kitongoji baina ya Kijiji
cha Mafisa wilayani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda
Kashai amemtaja aliyefariki dunia kwenye tukio hilo kuwa ni Lokoye Machaku (29)
kabila Mnguu mkazi wa Mafisa wilayani humo ambapo alichomwa kwa kitu chenye
ncha kali sehemu mbalimbali kwenye mwili wake.
Aidha amesema kuwa wakati huo mtu
mwengine aliyekuwa ameongozana na marehemu Mohamed Mhina (35) mkazi wa eneo
hilo alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika mkono wake wa
kulia.
Kamanda Kashai amesema kuwa tukio
hilo lilifanywa na watu wawili wa jamii ya wafugaji na walikuwa wamevaa nguo za
kimasai na inasadikiwa kuwa ni wakazi wa kijiji cha Lembapuri wilayani Kiteto
mkoani Manyara.
Amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo
ni kugombania malisho ambapo watuhumiwa walilisha mifugo yao mabua yaliyokuwa
shambani baada ya mavuno katika eneo hilo la mafisa.
Hata hiyo amesema kuwa mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kilindi kwa ajili ya
uchunguzi wakati jeshi hilo linaendelea na msako mkali kuwatafuta wahalifu
waliohusika kwenye tukio hilo.



0 comments:
Post a Comment