photo tyyyyyyyyyyyyyyyy_zpsd20272cf.jpg

SIMBA KUKIPIGA NA ORLANDO PIRATES MECHI YA KIRAFIKI< WAKIJIANDAA NA MCHEZO NA WATANIA WAO YANGA

KOCHA WA SIMBA SC>PATRICK PHIL

SIMBA SC keshokutwa (Jumamosi) itacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji Orlando Pirates mjini Johannesburg, Afrika Kusini katika sehemu ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam.

Katika mchezo huo, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenao kuanzia Jumatatu.

Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki.
Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.

Simba SC imefikia katika hoteli ya Eden Vale Petra na itakuwa inafanya mazoezi kwenye viwanja wa Eden Vale mjini Johannesburg.

Msafara wa kwanza Simba SC uliondoka jioni ya jana kwa ndege ya Fast Jet ukiongozwa na kocha Mkuu, Mzambia Patrick Phiri- wakati kocha wa makipa, Iddi Pazi ‘Father’ ameachwa Dar es Salaam.
EMMANUEL OKWI

Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.

Itakumbukwa Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment