Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi, Watendaji katika ngazi zote Tarafa, Kata, Mitaa, Vijiji na
Vitongoji, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya Siasa wameagizwa kuonyesha
ushirikiano katika kuhakikisha jukumu la
utambuzi na usajili wa watu linaenda sawasawa na maagizo ya Serikali .
Msisitizo huo umetolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ambaye ameahidi kutoa ushirikiano
wakati akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu uliofanyika mapema
leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu. |
| Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima ( Alhaji) akizunguza muda mchache kabla ya uzinduzi. |
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho( NIDA) Bw. Joseph Makani amewataka wakazi wa Tanga kujitokeza
na kutoa ushirikiano katika zoezi zima kwani zoezi hilo Mkoani Tanga ni utekelezaji wa Mpango wa
Usajili wa Wakazi waishio Kihalali Nchini kwa lengo la kuwapatia vitambulisho
vya Taifa kwa hadhi ya raia, Wageni wakazi na Wakimbizi.
| Baadhi ya viongozi wawakilishi kutoka katika Wilaya za Tanga wakati wa uzinduzi Huo |
“Fichueni wale ambao
hawastahili kupata vitambulisho vya uraia kwa kutoa taarifa katika ofisi za
uhamiaji na polisi ili taifa lisije likaingia katika hatari ya kuwasajili
wageni kama raia”amesisitiza Makani.
hivyo Wananchi wanatakiwa wanajitokeza na kuhakikisha wanajisajili kwa wenyeviti wa mitaa ili kurahisisha zoezi hilo.



0 comments:
Post a Comment