photo tyyyyyyyyyyyyyyyy_zpsd20272cf.jpg

INTER MILAN ,KUSUKA AU KUNYOA MTOTO WA PELE AU MARSEILLE....?

Andre Ayew
INTER MILAN WAMTAKA MTOTO WA PELE, ILA MARSEILLE KUMUACHIA NDIYO SHUGHULI!

KLABU ya Inter Milan imefufua mango wake wa kutaka kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew.

Vyombo vya Habari Ufaransa vimeripoti kwamba klabu hiyo ya Italia inamfuatilia kwa makini wing huyo wa Ghana, Ayew (pichani chini) ambaye Mkataba wake unamalizika katikati ya mwaka 2015.

Nia ya ya kumsajili kiungo huyo wa Ghana kutoka klabu hiyo hii si mara ya kwanza, kwani amekuwa akihusishwa na mango wa kuhamia huko tangu mwaka 2011. Ayew hajawahi kuonyesha nia ya kuondoka Marseille.

Huku Liverpool na Newcastle nazo zikiwa kwenye orodha ya klabu zinazotajwa kumuwania mchezaji huyo pia, Ayew hawezi kuuzwa kwa dau la chini ya Euro Milioni 11.

Lakini chini ya kocha mpya, Marcelo Bielsa, mtoto huyo wa Abedi Pele ameanza kurudi kwenye kiwango chake na bila shaka itakuwa vigumu kwa klabu yake kumuachia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment