MKAZI mmoja wa kijiji cha Malolwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa,
Ndikile Sunguli (38) amejichoma ndani ya nyumba hadi kufa baada ya
kumjeruhi mke wake katika ugomvi unaoaminika ni wa mapenzi.
Tukio hilo la kutisha lilitokea Septemba 29, 2014 majira ya saa tano usiku katika kijiji cha Mlolwa.
Imeelezwa kuwa Sunguli alirudi kutoka matembezini akiwa amelewa huku
akipiga makelele, alipofika nyumbani kwake alianza malumbano na mke wake
huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaluanda alisema kuwa wakati
ugomvi ukiendelea Sunguli alichukua kisu na kumchoma mkewe wake ubavuni
na kumjeruhi.
Kamanda alisema kuwa katika harakati za kujiokoa mama huyo alianguka
nje ya nyumba yao na kuzirai, hali inayodhaniwa ilisababisha mume
kudhani ameua na kujifungia ndani na kuwasha moto akiwa ndani.
Alisema kutokana na nyumba hiyo kuezekwa kwa nyasi ilishika moto kwa
kasi na juhudi za majirani kumuokoa ziligonga mwamba kutokana na
kujifungia.
Kamanda Mwaluvanda alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri kwani alikimbizwa kituo cha afya Mpui baada ya tukio hilo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment