![]() |
| Wayne Rooney |
Kiungo mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney anajiamini
ataweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi timu yake ya
taifa, England kwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton.
Kwa sasa Rooney anashika nafasi ya nne kwa
kuifungia mabao mengi England 41, yakiwa matatu nyuma ya Jimmy Greaves, saba
nyuma ya Gary Lineker na nane nyuma ya Charlton mwenye mabao 49.
Kiungo huyo ambaye ana umri wa miaka 28
tu, ndiye Nahodha wa kikosi cha timu hiyo kwa sasa ambacho kitamenyana na San
Marino Uwanja wa Wembley usiku wa leo. "Ni wakati wangu sasa kuwapiku
wote. Najihisi naweza kabisa kufanya hivyo. Hiyo itakuwa heshima
kubwa,"amebainisha



0 comments:
Post a Comment