Waandamanaji wanaopigania demokrasia
katika eneo la utawala la Hong Kong nchini China "wamesikitishwa" japo
hawajashangazwa na hatua ya serikali ya utawala wa eneo la Hong Kong
kufuta mazungumzo na wanafunzi hao ili kutatua mgogoro uliotikisa eneo
hilo kwa karibu wiki mbili. Amedai mwanafunzi mmoja kutoka katika jiji hilo
.
Mwanafunzi
mwandamanaji Harold Li ameishtumu serikali kwa kushindwa kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo, ambao umeshuhudia maelefu ya watu wakiingia
mitaani kuandamana.
Hong Kong imewalaumu wawakilishi wa wanafunzi kwa "kupuuza" msingi wa kuwepo kwa mazungumzo yenye tija kati ya pande mbili hizo.



0 comments:
Post a Comment