Nchini England Manchester United walitoka sare ya goli 1 -1 na Vijana kutoka darajani Chelsea katika uwanja wa Old Trafford.
Haikuchukua
muda mwingi punde tu baada ya kuanza kwa kipute hicho, mchezaji mkongwe
Didier Drogba akawainua mashabiki wa Chelsea baad ya kufunga goli zuri
la kichwa.
Goli hili liliweza kudumu hadi dakika za nyongeza za
mchezo huo na kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuamini kuwa
wangekusanya point zote tatu kutoka kwa Man U.
Dakika ya 93 ya
mchezo Mholanzi Robin van Persie akawainua mashabiki wa timu yake pamoja
na kocha wake Louis van Gaal baada ya kuisawazishia timu yake kwa shuti
kali la guu la kushoto na kufanya matokeo kuwa ni sare ya 1-1 mpaka
kipyenga cha mwisho.
Baada ya kupata goli la dakika za lala salama
Kocha Louis Van Gaal hajafurahishwa na timu yake ya Manchester United
japokuwa vijana hao wa Old Trafford wameweza kuondoka na point moja
muhimu katika mchezo dhidi ya Chelsea uliochezwa katika dimba la Old
Trafford. '' hatujatumia faida ya kuwa nyumbani na tungeweza kushinda
mchezo huu'' alisema Mholanzi huyo.
Goli la kichwa la Didier
Drogba liliisaidia Chelsea kushika usukani katika mchezo huo kabla ya
Robin van Persie kusawazisha na kuwasaidia vijana



0 comments:
Post a Comment