TANZANIA inakabiliwa na upungufu wa wataalam wa upasuaji kwa watoto
wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo kwa sasa ina madaktari watano
ambao wanazunguka katika hospitali za rufaa nchini kutibu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa
na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk. Othman Kiloloma katika maadhimisho ya
siku ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kimataifa
Dk. Kiloloma alisema kwa kuwa tatizo la watoto wanaozal;iwa na
ugonjwa huo ni kubwa, wataalam wa kutibu tatizo hilo wanapaswa kuwa
wengi ili waweze kujigawa katika hospitali za rufaa ambazo zinatoa
huduma hiyo.
Alisema madaktari hao watano pamoja na wataamu wengine kutika nje ya
nchi, hutibu watoto 200 kwa mwaka, idadi aliyodaikuwa ni ndogo sana
kulingana na mahitaji.
“Ingawa hospitali za rufaa za MOI, KCMC na Bugando zinazotoa huduma
hii kupokea watoto wengi wenye tatizo hilo, bado watoto wengi wapo
vijiji …wanashindwa kuletwa kutokana na gharama kubwa za usafiri na
kujikimu wawapo wodini” alisema Dk. Kiloloma
Naye Daktari bingwa wa magonjwa hao, Hamis Shaban alisema watoto
wanaopata tatizo hilo, wengi wao uwa walelamavu wa miguu kutokana na
kukosa nguvu, wengine upata utapiamulo na kushambuliwa na magonjwa
tofauti kutokana na lishe wanayopata.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo
wazi, Abdulhakim Bayakub, alisema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya
100 upoteza maisha kila mwaka kutokana na wazazi wao kuhusisha ugonjwa
huo na imani za kishirikina.



0 comments:
Post a Comment