photo tyyyyyyyyyyyyyyyy_zpsd20272cf.jpg

WIZRA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YASEMA HAINA PESA,KUKOPESHA WANAFUNZI WOTE ELIMU YA JUU,,,,,,

WAZIRI WA EILIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MH:SHUKURU KAWAMBWA
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema haina fedha za kutosheleza kuwakopesha wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu na kusema imetoa Sh. bilioni 306 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. 

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Sylvia Temu, alisema serikali imekwishatoa Sh. trilioni 1.6 kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004.

“Tatizo kubwa, kuna changamoto ya fedha. Serikali haiwezi kukopesha wanafunzi wote wanaopeleka maombi HESLB. Tunaomba taasisi binafsi waunge mkono katika kuchangia elimu,” alisema Temu.

Aliwataka wadau, watu binafsi na taasisi mbalimbali katika sekta ya elimu kuchangia elimu kwa kushiriki kusomesha watoto.

Kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), wanafunzi walioomba mkopo ni 58,037 wakati bajeti iliyotengwa na serikali ilikuwa ni kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 tu mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment