photo tyyyyyyyyyyyyyyyy_zpsd20272cf.jpg

KINANA ATOA ELIMU KWA WALIMU KUHUSU HAKI ZAO......

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amewataka walimu kuondoa uoga katika haki zao kwa kuitwa wapinzani kwakuwa   wana haki ya kuzidai.

Kinana aliyasema hayo wilayani Kilolo, mkoa wa Iringa, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo, baada ya kupokea taarifa ya wilaya juu ya walimu kuidai serikali  madai  mbalimbali, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani hapa katika kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM.

 “Walimu wana haki kama watu wengine na wanapodai madai yao ya msingi wasikilizwe na juhudi za kuwalipa zifanyike, muache tabia ya kuwaita ni wapinzani wanapokuwa wanadai. Maana mnapoona wanadai tu mnaanza kusema hawa ni wapinzani, wapinzani wakati wanadai haki yao,” alihoji Kinana.

Alisema endapo walimu wakilipwa stahiki zao wataacha kuwa wakali, hivyo ni lazima walipwe haki hizo wanazodai.


Kinana alisema pamoja na serikali kuendeleza juhudi kubwa za kuwalipa walimu madai yao, wapo wadendaji wachache wanaoshiriki kula fedha za walimu.


“Unaweza ukakuta mwalimu wa watu malipo yake yameshatumwa siku nyingi lakini kuna mtendaji yamepitia kwake akaamua kuyachukua bila ya mhusika kufahamu. Na bila kujua mwalimu wa watu anaendelea kuidai serikali,” alisema Kinana.


Katika hatua nyingine, walimu wa shule mbalimbali katika wilaya hiyo, wamemtaka Kinana awasaidie kutokana na kukosekana kwa nyumba za walimu hali inayowalazimu kuishi kwenye nyumba za nyasi.


Aidha, wamelalamikia upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwamo chaki pamoja na upungufu wa madarasa, hali inayowalazimu wanafunzi kusoma kwa awamu. Mwalimu wa Shule ya Msingi Iwindi, Joyce Konga, alisema katika kijiji hicho hakuna nyumba za kupanga wala nyumba za walimu, hali inayowalazimu kuishi katika nyumba za nyasi.


Kutokana na malalamiko hayo, Kinana alilazimika kutembelea shule hiyo na kushuhudia madarasa mawili katika shule hiyo na moja likitumika kama ofisi na stoo na jingine kutumika kufundishia darasa la kwanza hadi la tano kwa awamu.


Ameuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanamaliza jengo hilo mwaka huu na apatiwe taarifa pindi litakapokamilika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment