photo tyyyyyyyyyyyyyyyy_zpsd20272cf.jpg

PSPF YATOA MIFUKO 250 YA SARUJI, KWA MKUU WA WILAYA YA MKINGA BI MBONI MGAZA,KATIKA JUHUDI ZAKE ZA KUISADIA JAMII KATIKA MASUALA YA MAENDELEO


PSPF YATOA MIFUKO 250 YA SARUJI, KWA MKUU WA WILAYA YA MKINGA BI MBONI MGAZA,KATIKA JUHUDI ZAKE ZA KUISADIA JAMII KATIKA MASUALA YA MAENDELEO

MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza ametoa shukurani zake kwa  Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) kwa kusaidia sekta ya elimu wilayani humo lengo likiwa kupatikana kwa elimu bora na yenye tija kwa kizazi hiki chenye ushindani katika soko la ajira na maendeleo makubwa kiteknolojia.

  Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akipokea msaada wa  mifuko 250 ya saruji yenye thamani ya sh.milioni nne kutoka kwa mfuko huo wa Pensheni katika makabidhiano yaliyofanyika shule ya msingi Mwakikonge ya jamii ya kimasai wilayani humo.

Mfuko huo wa Pensheni ulitoa mifuko hivyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kwenye shule tatu za msingi wilayani humo ambazo zinakabiliwa na changamoto hiyo ambazo ni Mwakikonge mifuko 100,Mwakikoya mifuko 100 na Gonja Segoma mifuko 50.

Alisema juhudu hizo zinaonyesha kuwa namna gani mfuko huo ulivyokuwa  na malengo makubwa ya kuhakikisha wanachangia maendeleo ya sekta hiyo hasa katika masuala ya ujenzi wa miundombinu jambo ambalo linasaidia kukuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hizo.

Aidha alisema kuwa wilaya hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila shule inakuwa na miundombinu ya kutosha ikiwemo madarasa ilikuwawezesha wanafunzi kusoma kwa

Aliongeza kuwa shule hiyo ya Mwakikonge ina uhaba mkubwa wa
miundombinu ambayo ilijengwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuwasaidia jamii ya kimasai ili kuweza kupata elimu na kuwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jihudu hizo.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi mifuko hiyo,Afisa wa Fedha wa  Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Samweli Haule alisema kuwa waliamua kutoka msaada huo ili kuchangia harakati za elimu wilayani humo kwa kuboresha miundombinu.

Aliongeza kuwa baada ya kutoa msaada huo matumaini yao makubwa ni  kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora ambayo inaweza kuwainua kiwango cha ufaulu wao hasa katika mitihani yao ya mwisho.

Akitoa shukurani zake,Afisa elimu Msingi wilayani Mkinga,Zakayo  Mlenduka alisema msaada huo umewafikia wakati muafaka ambapo walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu na kuhaidi kuutumika kwenye matumizi yasiyokusudiwa.

Utoaji wa mifuko hiyo ya Saruji katika shule hizo unatokana na ombi  ambalo liliwasilizwa kwenye mfuko wa PSPF na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantuma Mahiza kuwaomba wasaidie masuala ya ujenzi kwenye shule ya mwakikonge inayotumiwa na jamii ya kimaasai ili waweze kupata elimu bora na stahiki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment