Ureno imekubali kipigo cha 2-1
katika mchezo wa kirafiki wa kimatafa, ambao Mwanasoka Bora wa Dunia Cristiano
Ronaldo hakuumaliza baada ya kuumia.
Mnamo dakika 76 ya mchezo Ronaldo alitolewa nje baada ya kuumia goti , wakati huo Ufaransa inaongoza kwa mabao 2-0.
Mabao ya Ufaransa yamefungwa na mchezaji mwenzake wa
Real Madrid, Karim Benzema dakika ya tatu na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba dakika ya 65.
bao lakufutia machozi limefungwa na Ricardo Quaresma aliyetokea benchi mnamo dakika i dakika ya 78 kwa njia ya penalti.



0 comments:
Post a Comment