Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Mhe
Jaji Mshibe Ali Bakar ameitaka jamii kuacha kukimbilia mahakamani kwa
ajili kupeleka mashauri kuwa kesi nyingi ambazo zinafikishwa mahakamani
zinaweza kutatuliwa nje ya mahakama .
Amesema kuwa Tume hiyo imeamua kutembelea maeneo yote ya Zanzibar kwa lengo la kutoa taaluma kwa jamii juu ya sheria ili kusaidia kupungua kwa mrundikano wa kesi mahakamani ambazo baadhi zinakosa ushahidi .
Akizungumza na katika kikao kilichowashirikisha wananchi kutoka taasisi za Serikali na Binafisi Mkoa wa Kaskazini Pemba , Jaji Mshibe amesema kuwa mwananchi anayetaka kupeleka sheuri mahakamani hanabudi kujitambua kabla ya shauri lake hajalifikisha mahkamani .
Katika hatua nyingine Jaji Mshimbe amesema kuwa jamii inahitaji kubadilika ili kurejesha suala la uaminifu ambalo linaonekana kupungua kwa wazee Kisiwani Pemba hususani katika Wilaya ya Wete kutokana na kuongezeka kwa matendo maovu .
Akichangia katika Kikao hicho Sheha wa Shehia ya Mtemani Wete , Juma Mrisho Magogo amesema kuwa bado baadhi ya wazazi wanawaonea haya watoto wao na kwamba wanashindwa kuzungumza na kuwakemea ili wasijihushe na matendo maovu .
Amefahamisha kuwa iwapo jamii itakuwa tayari kuwakemea watoto wao pamoja na jirani zao , ni dhahiri kuwa mrundikano wa kesi mahakamani utapungua na mahakimu kuweza kushughulikia chache na ambazo zinaushahidi uliokamilika .

0 comments:
Post a Comment