Wanaojadili maswala haya ni viongozi wa kanisa hilo na wanatarajiwa kufanya
hivyo kwa uwazi bila uoga wowote.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Vatican, David Willey anasema kuwa Papa
alifungua mkutano huo na kuwataka viongozi hao kuongea bila uoga wowote kwa
kipindi cha wiki moja.
Papa alianzisha mjadala wa baadhi ya mambo ambayo ni mwiko kwa wengi wa
viongozi wa kanisa na kuwataka kuyajadili bila uoga.
Aliwaambia zaidi ya viongozi 200 wa kanisa hilo pamoja na wataalamu kuongea
bila hofu ya kumuudhi , kuongea ukweli na kwa uwazi na kusikiliza kwa umakini.
Mkutano huu ni wa kipekee kwani mikutano ya Vatican kwa kawaida huwa na kimya
kingi.
Lugha ambayo hutumika kwa kwaida huwa imejaa maneno yanayoambatana tu na
mafunzo ya kanisa.
Papa Francis alifungua rasmi mkutano huo na kuwataka viongozi wengine
kuongea kwa uwazi. Papa amekuwa akitaka gumzo katika kanisa kuhusiana na
maswala ya ngono na pengo lililopo katika mafunzo ya dini na masuala kuhusu
familia na ambavyo familia za kikatoliki zinaishi maisha yao.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu ikiwa ni sawa
kuruhusu wakatoliki wanaotalakiana na kisha kuona tena kukubaliwa kupokea
sacramenti.
Papa Francis anataka kanisa kuwaonea huruma watu waliotalakiwa bila ya
kulegeza msimamo kuhusu maswala ya ndoa.



0 comments:
Post a Comment